Maelezo ya kina kuhusu sera za kazi na hali iliyoko nchini Saudi Arabia yawezapatikana hapa. Kulingana na habari hii na vyanzo vya ziada, vidokezo vifuatavyo kwa watu binafsi walio na nia ya kuhamia Saudi Arabia vinaweza ratibiwa;

  • Usiende Saudi Arabia bila idhini ya awali kutoka kwa Wizara ya Leba na ile ya Ndani nchini Saudi Arabia.
  • Usiende Saudi Arabia kabla ya kupata mdhamini rasmi, raia ya Saudi Arabia ama kampuni ya kimataifa.
  • Usiende Saudi Arabia bila kibali halali cha kazi na kadi ya makazi (iqama).
  • Usilipe ada za kuajiriwa kwa mashirika ya Saudi Arabia kabla ya kuondoka nchini mwako.
  • Hakisha umetia saini kandarasi ya kazi iliyo kwa Kiarabu ikifafanua haki zako kulingana na sheria za kazi nchini Saudi Arabia na muda wa ajira.
  • Kiwango cha juu zaidi cha muda wa kufanya kazi kila wiki hakifai kuzidisha masaa sitini (60) ikiwa ni pamoja na muda wa ziada (overtime). Ingawa kuna ratiba maalum kwa wakati mwingine.
  • Ijumaa (Friday) ni siku ya mapumziko kwa kila mfanyikazi.
  • Saudi Arabia haina kiwango kamili na rasmi cha malipo.

Wizara ya Mambo ya Nje ina wajibu wa kushughulikia mambo yanayohusu visa, ikiwemo kazi na visa ya makazi.

Mwongozo unaolenga wafanyakazi wenye ujuzi wa kati na wa chini ni nadra, angalau kwa lugha ya Kiingereza. Mwongozo kutoka kwa shirika la kimataifa la wafanyikazi (ILO) kwa wafanyakazi wahamiaji kutoka Pakistan na ule wa wafanyakazi wahamiaji kutoka India wafanyaokazi nchini Saudi Arabia, uliochapishwa na kamati kuu ya Uhindi, inatoa maelezo yanayowalenga wafanyakazi wahamiaji wenye ujuzi wa kati na wa chini ambayo ni ya umuhimu kwao kabla ya kutoka nchini mwao na pindi wanapowasili Saudi Arabia. Pia ni ya umuhimu kulingana na sheria na masharti, uwezekano wa hatari na utaratibu wa kuzipunguza, maelezo kuhusu njia za mawasiliano iwapo kuna matatizo.

Vivyo hivyo, miongozo muhimu imo kwa kundi la wafanyakazi Wafilipino ugenini lijulikanalo kama Overseas Filipino Workers (OFW) ; miongoni mwa mingine, kuna mwongozo kwa mfumo wa Kafala (udhamini), mwongozo unaotoa maelezo na habari za jumla kuhusu Saudi Arabia kwa OFW, na kushauri kuhusu kutambua mashirika ama waajiri wasio wa kisheria.