Maelezo yafuatayo ni ya kijumla kuhusu makubaliano ya nchi mbili ambayo Saudi Arabia imetia saini.

Ufilipino, 2013 makubaliano kuhusu kuajiri wafanyakazi wa nyumbani; kulinda haki za waajiri wa Saudi Arabia pamoja na wafanyakazi wa nyumbani kutoka Ufilipino na kudhibiti uhusiano wa mikataba kati ya hao wawili. Inajumuisha masharti ya kuhakikisha kuajiri, kukodisha na kuwekwa kwa wafanyakazi wa nyumbani kumefanywa kwa mujibu wa sheria, masharti na kanuni husika.

India, 2014 makubaliano kuhusu ushirikiano wa kazi kuhusu uajiri wa wafanyakazi wa nyumbani; kupunguza uhaba wa wafanyakazi wa nyumba. Inajumuisha masharti ya kuhakikisha uhalali na utekelezaji wa mkataba wa ajira wa kawaida, gharama ya kuajiri, hatua dhidi ya mashirika ya kuajiri yanayokiuka sheria na utaratibu wa kuzuia kudanganya kwa madalali; Inatoa kiwango cha chini zaidi cha mshahara, masaa ya kazi, likizo za kulipwa na utaratibu wa kutatua migogoro kazini.

Indonesia, 2014 makubaliano ya uwekaji na ulinzi wa wafanyakazi wa nyumbani kutoka Indonesia; kuanzisha utaratibu wa ufanisi wa uwekaji wa wafanyakazi wa nyumbani kutoka Indonesia, kuhakikisha ulinzi wa haki zao na za waajiri wao na kuweka mkataba halisi wa ajira.

Sri Lanka; mkataba wa makubaliano kati ya nchi mbili kuhusu wafanyakazi wa nyumba.

Vietnam, Nepal, Niger, Djibouti, Bangladesh na Chad 2016; mikataba kati ya nchi mbili kuhusu wafanyakazi wa nyumba.