Maelezo yanayofuata ya sheria za taifa yana maana kwa wafanyakazi wahamiaji yakiwa ni pamoja na masharti yanayodhibiti uajiri wa wafanyakazi wahamiaji na hatua kwa ajili ya kuwalinda (kwa mfano; mafunzo ya awali kabla ya kuondoka nchini mwao, mipango ya bima na kadhalika.):

Uamuzi wa Baraza Na. 166 wa Julai 12, 2000 kuhusu kanuni za uhusiano kati ya waajiri na wa fanyakazi wa kigeni; Husema kwamba uhusiano kati ya waajiri na wafanyakazi wa kigeni utadhibitiwa na kandarasi ya ajira iliyokamilishwa kati yao wala sio sheria za udhamini. Husema pia kwamba wafanyakazi wa kigeni watawajibika kwa kuhakikisha ombi lifanywe kwa idara ya pasipoti ili kupata kibali cha makazi yao pamoja na familia.

Amri ya Baraza la Mawaziri Na. 257, Novemba 13, 2006; yasema kwamba kiasi cha 1,000 ya Saudi Ryal (Shilingi 27, 000 ya Kenya) zilipwe kwa kila kibali cha makazi cha Saudi Arabia.

Amri ya Kifalme M/73 ya usajili 17/11/1436H; Inadhibitisha visa za kisasa na misimu.

Amri ya Kifalme kuweka ada ya 1,000 Ryal ya mfanyakazi kubadilisha ajira; Kuweka ada ya 1,000 ryal mfanyakazi wa kigeni kubadilisha ajira.

Kanuni za Amri kuu za Kifalme Na. 17/2/25/1337 na 11/09/1371H (4//6/1952G) kuhusu makazi; Hudhibiti kuingia, kukaa na kutoka kwa wageni nchini Saudi Arabia.