Moja ya changamoto muhimu zaidi kuhusu Saudi Arabia ni ongezeko la kuhitajika kwa wafanyakazi wa nyumbani. Hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa kuajiriwa kwa wafanyakazi wahamiaji; kulingana na wanauchumi wa Saudi Arabia, ufalme huu huajiri takriban milioni 1.2 ya wanyakazi wahamiaji ilhali zaidi ya milioni moja wa raia wa Saudi hawana ajira. Kwa kweli, raia hao huchukua 15% tu ya nafasi zilizoko katika sekta binafsi, kisa kinachosababisha wanauchumi na wataalam kuomba serikali kuangalia tena kwa uchambuzi sera za kuajiri. Sababu kamili ni kwamba wafanyakazi wahamiaji huenda wakakubali kufanya kazi kwa masaa zaidi na kwa malipo ya chini zaidi ukilinganisha na raia wa Saudi Arabia. Hivyo basi, kampuni za kibinafsi hupendelea kuajiri wafanyakazi wahamiaji.

Chanagamoto nyingine kuhusu kuajiri nchini Saudi Arabia huhusiana na kuajiriwa kwa wafanyakazi wahamiaji walio na ujuzi mdogo kutoka nchi kama Pakistan, Bangaladesh, India, Indonesia na kadhalika na hatari amabazo huwakumba. Wakati waajiri wa wafanyakazi wahamiaji walio na ujuzi wa juu hugharamia ada za kuwaajiri, wafanyakazi wahamiajia walio na ujuzi mdogo katika ujenzi, kilimo na huduma nyinginezo (ikiwa ni pamoja na kazi za nyuambani) huegemea mashirika ya kibinafsi kwa kupata usaidizi. Kwa wastani, gharama hizo hufikisha hadi $3,500 kwa kila mfanyakazi mhamiaji, ikiwa ni pamoja na takriban $2,300 ya visa, $350 ya usafirishaji wa kimataifa na $245 ya mawakala. Jumla ya gharama hizo hivyo basi ni kiasi cha mishara ya miezi kadhaa ya hawa wafanyakazi.

Sheria za kazi za Saudi Arabia huzuia kutozwa kwa ada dhidi ya wafanyakazi, lakini mashirika ya kuajiri hutafsiri hizo kuwa ni kuzuia kwa kukatwa kwa mishahara katika nchi za kigeni, na kwa hiyo, ada hizo hutozwa kabla ya kuondoka nchi za asili.

Miongoni mwa wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya chini, wanawake hukabiliana na hatari zaidi. Wengi wa wanawake ambao ni wafanyakazi wahamiaji na wa kazi za nyumbani katika majimbo ya Kiarabu huajiriwa kutoka Indonesia, Bangladesh, Sri Lanka, India, Nepal, Ufilipino na Ethiopia. Kulingana na utafiti wa hivi karibuni, sehemu kubwa ya wanawake wanaofanya kazi Saudi Arabia kutoka Bangladesh wanadaiwa kuwa wamechukuliwa na kushughulikiwa kama mtumwa wa kisasa, kwa kukabiliwa na uzoefu wa kuchelewa kwa mishahara na kupokonywa pasipoti.

Ili kukabiliana na ongezeko kubwa la kuhitajika kwa wafanyakazi wa nyumbani, pia ongezeko la kuajiriwa kwa wafanyakazi wa kigeni na changamoto zinazojiri; kama gharama za juu za kuajiri na unyanyasaji, Wizara ya Leba nchini Saudi Arabia imeidhinisha afisi mpya za kuajiri wafanyakazi wa nyumbani. Wizara hii kwa hivyo inatarajia kuongeza na kuinua ushindani na kupunguza gharama. Zaidi ya hayo, wizara hii pia iliamilisha wa mfumo wa kuajiri kidigitali katika tovuti unaoeleza kuhusu hali ya kazi na mahitaji ya afya na usalama na pia kusema kwamba kandarasi ziwe kwa lugha zinazoeleweka kwa wafanyakazi.

Kulingana na mapendekezo ya shirika la kimataifa la wafanyikazi (ILO), Saudi Arabia ni miongoni mwa mataifa ya marudio ambayo yanafaa kuzingatia utaratibu wa kukabiliana na biashara ya visa na kurahisisha utaratibu wa uhamiaji na tabaka mbali mbali za uhamisho, na haswa, gharama hizo.

Pata mengi kuhusu kiwango cha heshima kwa haki za wafanyakazi katika nchi kulingana na ripoti kadirio kuhusu haki za kimaitaifa (ITUC Global Rights Index) hapa.