Thibitisha hali ya shirika lako la kuajiri!

Angalia kama hilo shirika la kuajiri limeidhinishwa na Mamlaka ya Ajira ya Kitaifa, kabla ya kuendelea na mchakato wa kuajiriwa. (the National Employment Authority (NEA))

Fanya utafiti wako!

Fikiria kuchukua faida ya huduma zinazotolewa na NEA (services offered by the NEA) kwa ajili ya kutafuta ajira ugenini na mafunzo, yakiwemo huduma za ushauri wa mambo ya ajira, usaidizi katika uwekezaji wa ajiri na mafunzo, thibitisho za nafasi za ajira ugenini na mafunzo ya awali kabla ya kuondoka nchini. Mfumo wa habari za soko la ajira nchini Kenya (Kenya Labour Market Information System (KLMIS)) pia unatoa maelezo na rasilimali kwa upande wa ushauri wa kazi, kuandika mtaala (CV), kutafuta kazi na mbinu za mahojiano.

Hakikisha uko na mahitaji ya lazima!

Angalia mahitaji ya lazima kwa uhamiaji wa kazi kutoka kwa NEA (pre-requisites for labour migration from the NEA) yakijumuisha pasipoti ya Kenya, cheti asili cha kuzaliwa, hati ya kibali kutoka kwa polisi, mkataba halali wa huduma, cheti cha matibabu, kibali cha kazi na visa ya kusafiri. NEA hutoa miongozo kuhusu mahali na jinsi ya kupata mahitaji hayo ya lazima.

Tia saini katika mkataba halali wa kazi!

Soma mkataba wako kwa makini kabla ya kutia saini. Jadili masharti ya mkataba. Weka nakala moja ya mkataba. Usitie saini mkataba usioelewa au usiokubaliana nao. Kabla ya kufanya kazi ugenini, Wakenya lazima pia wawe na mkataba wao wa kazi kuthibitishwa; huduma za uthibitishaji zinatolewa katika Idara ya Leba (Department of Labour).

Jua haki zako!

Pata kujua Zaidi kuhusu Sheria za Leba za nchi uendako. Kuwa na rekodi muhimu za njia za mawasiliano za serikali na chama cha wafanyakazi iwapo utakumbana na shida za kuajiri au kazi.

Chama cha kutetea wafanyakazi cha KUDHEIHA, chenye ushirikiano na Shirikisho Kimataifa la Wafanyakazi wa Nyumbani (International Domestic Workers Federation – IDWF), kimekuwa kikifanya na manusura na wafanyakazi wa nyumbani waliookolewa, ili kushiriki kwa kutoa maelezo ya hali na uzoefu wao katika kuwatayarisha wafanyakazi wa nyumabni wa siku zijazo. Kudheiha pia inatoa mpango wa mafunzo ya kitamaduni ya kuwaandaa wafanyakazi kwa ujuzi muhimu wa kuwasili ugenini. Kudheiha pia inaweka wafanyakazi katika mpangilio na kuimarisha sheria za kikazi nchini Kenya, na kushughulikia mianya iliyoko katika sheria za uhamiaji, ikiwemo kampeni za kushinikisha serikali kuthibitisha Mkataba wa kimataifa wa wafanyakazi wa nyumabani (ILO C189).

MAELEZO NMENGINE MUHIMU