Maelezo yanayofuata ya sheria za taifa yana maana kwa wafanyakazi wahamiaji yakiwa ni pamoja na masharti yanayodhibiti uajiri wa wafanyakazi wahamiaji na hatua kwa ajili ya kuwalinda (kwa mfano; mafunzo ya awali kabla ya kuondoka nchini mwao, mipango ya bima na kadhalika.):

MWAKA

SHERIA

MAELEZO

2007

Sheria ya Taasisi ya Kazi

 

Sehemu za 55 – 60 zinaeleza masharti yanayoongoza mashirika ya kibinafsi ya kuajiri nchini Kenya. Haya ni pamoja na: i). Usajili na vibali kutoka kwa Wizara ya Leba.  ii). Wajibu wa anayeendeleza makampuni ya kuajiri na kuweka rekodi na yasiwatoze wanaotafuta kazi ila kwa yale yaliyoidhinishwa na sheria. Dhamana ya usalama unawezahitajika kwa waajiri/makampuni, Sh. 500,000 (USD 4,816). Chini ya ongezeko la ziada Nambari 92 katika Kenya Gazette, Ilani ya kisheria Na. 110 wa 17/06/2016. iii). Mamlaka ya maafisa wa kuajiri kufanya ukaguzi kwa hayo mashirika. iv). Makosa – yeyote asiyezingatia sheria hii anafanya kosa na anajibika kwa faini isiyozidi Sh. 50,000 (USD 480) au kifungo cha hadi miezi mitatu au yote mawili.

2007

Sheria ya Ajira

Sehemu za 83 – 86 za Sheria ya Ajira zinaeleza jinsi mikataba ya kigeni itashughulikiwa zikieleza kwamba: i). Mikataba yote itathibitishwa na afisa wa leba katika kikao kikuu cha Wizara. ii). Mikataba hiyo lazima ikidhi mahitaji ya kuhakikisha kwamba hakuna udanganyifu, kulazimishwa au ushawishi usiofaa. iii). Dhamana kwa usalama unawezahitajika kwa waajiri/makampuni, Sh. 500, 000 (USD 4,816) kwa sasa. iv). Kuwashawishi Wakenya kuenda ugenini bila mkataba halali ni kosa.

2010

Sheria ya kukabiliana na biashara ya usafirishaji wa binadamu.

Usafirishaji wa binadamu ni kosa la jinai. Sehemu ya 5(c) ya sheria hii inaeleza kuwa mtu yeyote anayewezesha, endeleza au dhamini kampuni la kuajiri kwa minajili ya usafirishaji wa binadamu anafanya kosa la jinai na anajibika kifungo cha muda usiopungua miaka ishirini au faini isiyopungua milioni ishirini (USD 192,678) au kwa yote mawili, kifungo cha maisha kwa uamuzi wa baadaye.

2014

Kanuni (za jumla kwa) Taasisi za Kazi

Ili mtu kuthibitishwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuajiri lazima awe raia wa Kenya au awe na kibali rasmi cha kazi; awe amehitimu na kufikisha cheti cha kiwango cha sekondari; na awe na diploma katika usimamizi wa rasilimali za binadamu (HRM). Lazima alipe USD 300 ya leseni kila mwaka, awe na hati ya mwenendo mzuri kutoka kwa polisi na kutoa dhamana ya USD 3,500 (umiliki wa Mkenya) au USD 10,600 (umiliki wa asiye Mkenya) na awe mwanachama cha ushirikiano wa mashirika. Hati kibali hupatikana upya kwa USD 2,650 (uwekezaji wa kigeni) na USD 1,325 (uwekezaji wa ndani). Gharama za uhamiaji zinapaswa kushughulikiwa na mashirika na waajiri, zikiwemo ada za visa, nauli za ndege na uchunguzi wa matibabu. Makampuni yanakubaliwa kutoza ada za huduma kutoka kwa mkuu ugenini (kwa mfano shirika la uwekezaji au mwajiri katika nchi uendako) ili kugharamia uajiri. Iwapo wakuu hawalipi, basi makampuni wanapaswa kulipisha kiwango sawa na mshahra wa mwezi mmoja kwa mfanyakazi. Lazima waingie katika mkataba uliowekwa na makampuni yaliyo na wajibu wa kuhakikisha kwamba wafanyakazi na waajiri wanatia saini. Makampuni yote yanapaswa kufuatilia ustawi wa waajiriwa wao. Makampuni yanahitajika kuwa wenye chama cha Vyumba vya Kitaifa vya Biashara (National Chambers of Commerce) na Shirikisho la pamoja la Vyumba vya kitaifa  vya Biashara la  Kenya na Kiarabu.

2016

Sheria ya Mamlaka ya Ajira ya Kitaifa

Sheria hii ya bunge ni ya kuzindua  Mamlaka ya Ajira ya Kitaifa; kutoa mfumo wa taasisi kamili kwa usimamizi wa ajira; kuboresha na kuongeza upatanisho katika uajiri; kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana, walio wachache na makundi yaliyo na upungufu na kwa malengo ya kushikamana.

Sources: Natlex