Uhamiajii wa ajira kutoka Kenya umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, badiliko ambalo limeashiria ongezeko katika ukubwa wa sekta ya ajira nchini tangia miaka ya 1990. Kadirio la Wakenya milioni tatu hufanya kazi ugenini, wengi wao wakikalishwa na nchi nyingine za Afrika kama Botswana, Ghana, Namibia na Tanzania. Ongezeko la uwiano wa wafanyakazi raia wa Kenya pia wanasafiri kuenda nchi za Mashariki ya Kati (kwa mfano Qatar, Saudi Arabia, UAE, Bahrain, Kuwait, Oman) kwa ajira za muda katika sekta za usalama, vifaa na zile za rejareja. Kuongezea, nyingi za nafasi hizi za kazi katika Mashariki ya Kati ni za kazi za nyumbani, au kujaza nafasi za kazi katika viwanda vya ujenzi na vya huduma kwa maandalizi ya maonyesho ya UAE (2020) na Kombe la Dunia la mwaka wa 2022 nchini Qatar. Katika suala hili, inakadiriwa kuwa wafanyakazi wahamiaji kutoka Kenya kati ya 100,000 na 300,000 wamo katika nchi za Guba.

Kuanzia miaka ya 2000, Kenya imefanya juhudi za kuanzisha sera za uhamiaji wa wafanyakazi kutoka Kenya ili kudhibiti uhamiaji kutoka Kenya na kupata nafasi za ajira kwa raia zake ugenini. Kumekuwa hasa, pia na majaribio ya kuzuia uhamiaji wa ajira katika nchi za Almashauri ya Ushirikiano wa Guba (Gulf Cooperation Council – GCC) na kuzuia usafirishaji wa wanawake kuenda Guba. Hata hivyo, serikali ya Kenya haina mikakati pana (kwa mfano makubaliano ya utendajikazi kati ya nchi mbili, sera za ustawi) ili kulinda haki za Wakenya wanaofanya kazi ugenini, kukabiliana na makosa ya mashirika ya kuajiri na kuunga mkono mchango wa kiuchumi wa walio ugenini. Zaidi ya hayo, sera ya uhamiaji ya serikali imebakia katika nakala rasimu. Juhudi za kuzuia unyonyaji kazini, hasa katika nchi za Guba, hazina ufanisi katika kiasi kikubwa. Kwa sababu za ripoti ibuka kuhusu unyanyasaji kazini unaowakumba wafanyakazi katika Mashariki ya Kati, serikali ya Kenya ilipiga marufuku uhamiaji wa kazi kwa nchi za GCC mnamo mwaka wa 2012. Hata hivyo, marufuku ilibatilishwa muda mfupi baadaye, kuripotiwa kuwa ni sababu za juhudi za mashirika ya kuajiri ya Kenya.

Kwa vile serikali ya Kenya imetatizika katikajuhudi za kudhibiti sekta ya kuajiri wafanyakazi, mashirika ya kuajiri mara nyingi hujiingiza katika ustawi wa unyanyasaji, vurugu na ukiukwaji wa haki za kibinadamu dhidi ya wafanyakazi wahamiaji. Matendo ya kuajiri kinyume cha sheria na yasiyo na maadili yakijumuisha kwa mfano, gharama za juu za kuajiri na hali za kushikamana na madeni bado ni ya kawaida. Kuongezea, wafanyakazi pia wanawezadanganywa na waajiri kuhusu sheria na masharti ya kazi fulani ama kupotoshwa na kazi bandia katika nchi waendako. Mafunzo ya awali kabla ya kuondoka nchini yaliyo madogo au yasiyo sahihi kutoka kwa mashirika ya kuajiri yanaonelewa kuwazuia wahamiaji kufahamu haki zao kikamilifu katika hali mbaya za kazi ugenini. Katika suala hili, malalamiko ya kina yamewasilishwa kutoka hizo nchi, hasa UAE. Katika nafasi za ujuzi mdogo, Wakenya wamo hatarini kwa unyonyaji na ukiukwaji unaohusiana na, kwa mfano, kupunguzwa kwa ujuzi, ugeuzwaji wa mikataba ya kazi, kukosa mishahara au ukatwaji usio wa kisheria, masaa marefu ya kazi na kuzuiliwa kwa pasipoti. Usafirishaji wa binadamu, dhuluma za kimwili na kimapenzi pamoja na utumishi, pia yameripotiwa miongoni mwa wafanyakazi raia wa Kenya (hasa wafanyakazi wa nyumbani) ugenini. Vifo vya Wakenya wa kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia pia vimeripotiwa, kwa mfano. Kwa sababu za hisia za kutoaminiana na mawazo ya ufisadi ndani ya ubalozi wa Kenya, wafanyakazi wahamiaji mara nyingi huvunjika nyoyo katika kuripoti na kutafuta usaidizi kulingana na ukiukwaji mikononi mwa mashirika ya kuajiri na/ama waajiri.

Pata mengi kuhusu kiwango cha heshima kwa haki za wafanyakazi katika nchi kulingana na ripoti kadirio za haki za kimataifa (ITUC Global Rights Index) hapa.