Sasisho, 1 September 2020: Kufuatia kupitishwa mnamo 30 Agosti 2020 ya Sheria Nambari 18 ya 2020, wafanyikazi wahamiaji sasa wanaweza kubadilisha kazi kabla ya kumalizika kwa mkataba wao bila kwanza kupata Cheti cha Kutokukataa (NOC) kutoka kwa mwajiri wao. Sheria ya nyongeza, Sheria Nambari 17 ya mwaka 2020, iliyopitishwa leo pia inaanzisha mshahara wa chini wa riyali 1,000 za Qatar (QAR) ambazo zitaanza kutumika miezi sita baada ya uchapishaji wa sheria katika Gazeti Rasmi. Mshahara mpya mpya utatumika kwa wafanyikazi wote, wa mataifa yote na katika sekta zote, pamoja na wafanyikazi wa nyumbani. Mbali na mshahara wa chini kabisa, waajiri lazima wahakikishe kuwa wafanyikazi wana makazi bora na chakula. Sheria hiyo pia inasema kwamba waajiri walipe posho ya angalau QAR 300 na QAR 500 ili kulipia gharama za chakula na makazi mtawaliwa, ikiwa hawapatii wafanyikazi hizi moja kwa moja - hatua ambayo itasaidia kuhakikisha viwango vya maisha bora kwa wafanyikazi. Chanzo: ILO

 

Maelezo yanayofuata ya sheria za taifa yana maana kwa wafanyakazi wahamiaji yakiwa ni pamoja na masharti yanayodhibiti uajiri wa wafanyakazi wahamiaji na hatua kwa ajili ya kuwalinda (kwa mfano; mafunzo ya awali kabla ya kuondoka nchini mwao, mipango ya bima na kadhalika.):

Uamuzi wa Waziri juu ya kukandamiza idhini ya kutoka. Ni muhimu kufafanua kuwa wafanyikazi wa nyumbani wanapaswa kuwajulisha waajiri wao ikiwa wanapanga kuondoka Qatar lakini hawahitaji ruhusa yao. Pata tafsiri ya Uamuzi No 95 ya 2019 na Waziri wa Mambo ya Ndani juu ya kanuni na taratibu kuhusu kuondoka kwa aina fulani ya wafanyikazi ambao sio chini ya Sheria ya Kazi hapa. Chanzo: ILO Qatar

Sheria Na. 13 wa 2018 inafanya marekebisho kwa Sheria No. 21 wa 2015 inayodhibiti kuingia na kutoka kwa wahamiaji na makazi yao; Kulingana na hii sheria, wafanyakazi wahamiaji wanaofunikwa na kanuni hizo za kazi wataweza kutoka Qatar bila kupata hicho kibali.

Amri ya Waziri No. 18 wa 2014 inayoamua mahitaji maalum ya makazi ya kutosha.

Amri ya Waziri wa Mambo ya Utumishi wa Umma na nyumba. Na. 8/2005 kuhusu udhibiti wa hali na utaratibu wa kutoa leseni kwa raia wa Qatar wanaotaka kuajiri wafanyakazi wahamiaji; utoaji wa leseni kwa raia hao ufanywe kulingana na sheria na masharti yaliyowekwa na hii amri.

Sheria Na. 23 wa 1994 kufanya masharti ya upatanisho katika uhusiano na makosa yaliyotolewa katika Sheria Na. 145 wa 1992, kudhibiti uingizaji wa wafanyakazi kwa mhusika wa tatu; Inatoa upatanisho kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa idara ya leba iwapo moja kati ya yale makosa yaliyotajwa, ama kabla ya taasisi ya kesi za kisheria au wakati kesi hizo zinapoendelea.

Sheria Na. 14, 1992, kudhibiti shughuli za mashirika ya kuagiza kazi kutoka nje. Iliunda mahitaji ya leseni ili kuleta wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar isipokuwa kwa wanaotaka kuleta watumishi wa nyumabani mwao wenyewe binafsi. Sheria hii hutoa masharti ambayo mashirika ya kuagiza kazi kutoka nje lazima yafikie ili kuhitimu kiwango cha kupata leseni (umri wa chini zaidi wa 21, dhamana ya benki na kadhalika) na kutoa dhana ya kuchunguzwa kwa stakabadhi zao na makazi yao. Masharika hayo hayakubaliwi kamwe kuwatoza ada raia wa kigeni wanaotafuta ajira ili kupewa nafasi za ajira. Gharama za usafiri na ada za juu za mashirika lazima zilipwe na mwajiri ambaye shirika lile huingiza ajira hizo kwa niaba yake. Mashirika yote yaliyoko na yanayoingiza wafanyakazi lazima yazingatie masharti ya Sheria Na. 19 wa Machi 1993.

Sheria Na. 7, 1992, kuthibitisha kanuni kuhusu kuajiriwa kwa raia wasio wa Qatar kwa wizara na idara za serikali; inatoa masharti na kanuni za kuajiri wageni kutoka nje, ikitaja kwamba upendeleo utapewa kwa walio na vibali vya makazi. Sura ya pili ya sheria hii inataja makundi ya kazi na viwango vinavyolingana na mshahara husika. Kanuni zinaundwa ili kulinda malipo; malipo ya nyakati za likizo, likizo wakati mfanyakazi ni mgonjwa (isiyozidi miezi sita) na faida za ulemavu, marupurupu ya nyumba, faida za kukamilika kwa huduma na kadhalika. Mikataba ya ajira inatumika katika kanuni hizo.

Sheria Na. 7, 1988, kutaja sheria zinazotumika kwa raia wa Majimbo ya Wanachama wa Halmashauri na Ushirikiano wa Ghuba (Member states of the Gulf Cooperation Council - GCC) wanaofanya kazi za kujitegemea nchini Qatar; inataja sheria zinazotumika kwa raia wa GCC waliojitegemea nchini Qatar.

Sheria Na. 2 of 1981, inayofanya marekebisho katika vipengee fulani vya Sheria Na. 34 wa 1962; Inarekebisha Makala 17(d) na 18(3) ya Sheria ya Leba Na. 3 ya 1962 inayosema kwamba iwapo mfanyakazi wa kigeni atasitisha ajira yake, basi atalazimika kuondoka nchini Qatar.

Sheria za Leba za Qatar, 2004; inatumika kwa raia na wageni nchini na kufafanua kanuni kuhusu mafunzo za kiufundi, ajira, malipo, masaa ya kazi na likizo pamoja na adhabu zilizoko kwa kukosa kuzingatia sheria hizo.