Kulingana na ripoti ya ILO, Qatar iko miongoni mwa nchi za GCC ambamo mikakati na mipango inayoendelea kuhusu miradi mikubwa ya miundombinu imesababisha mahitaji makubwa ya wafanyakazi walio na ujuzi wa chini. Zaidi ya 60% ya wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar hawajakamilisha masomo ya sekondari.

Qatar, kama nchi nyinginezo zilizowanachama cha GCC, uajiri wa wafanyakazi wahamiaji ni sekta kubwa. Bila kujali sheria, gharama za ajira wanazokabiliana nazo wahamiaji bado hazijadhibitiwa. Ongezeko na kukosa kudhibitiwa kwa gharama hizi huleta nafasi ya unyanyasaji na unyonyaji, miongoni mwa madhara mengine haramu.

Katika miaka ya 1990 na 2000, wengi wa wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar na nchi nyingine za GCC walitoka nchi za Kiarabu, siku hizi, wafanyakazi kutoka Asia wanaonelewa kuwa “watiifu zaidi”, “ wa gharama ya chini” na wa “kusimamiwa” kwa njia rahisi. Kuongezeka kwa kuitajika kwa wafanyakazi kutoka Asia pia inahusishwa na maoni ya kwamba hao uhama bila wategemezi, kinyume cha hali ya wafanyakazi Waarabu ambao huingia na familia zao na kulenga makazi ya kudumu. Maono kuhusu wafanyakazi kutoka Asia huathiri hali ya kuajiri. Kwa mfano, waajiri hutarajia wafanyakazi kutoka Ufilipino kuwa sahihi kwa nafasi za utawala kutokana na kuimarika kwao kwa lugha ya Kiingereza na sifa nzuri ya mashirika ya mafunzo nchini Ufilipino. Vile vile, Wapakistan huonelewa kuwa madereva wazuri, Wahindi kuhusishwa na kazi ya ujuzi, ilhali wafanyakazi kutoka Ethiopia, Vietnam na Cambodia hudhaniwa kuwa tayari kufanya kazi kwa malipo ya chini.

Nchi za GCC, ikijumuisha Qatar, kuajiri huelekezwa na mtindo wa Kafala (mdhamini), unaohitaji mfanyakazi mhamiaji kuwa na mdhamini aliyeidhinishwa. Kirasmi, Qatar imekataza kupokonywa kwa stakabadhi za usafiri, lakini wadhamini wengine huenda bado wanaitisha pasipoti za wafanyakazi wahamiaji. Ripoti ya ILO ya utafiti wa 2013 yaonyesha kwamba asilimia 90 ya wafanyakazi wenye malipo ya chini nchini Qatar walipokonywa pasipoti zao. Hii huzuia uhuru wa kusafiri kwa waathiriwa na kuwapa wadhamini nguvu zisizohalali dhidi ya wafanyakazi wahamiaji. Unyanyasaji na unyonyaji tofauti tofauti, madhara ya mtindo wa Kafala ni hatari zaidi kwa mfanyakazi wa ujuzi wa chini, hasa wanawake, kuliko wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya juu, hasa iwapo ni asili ya nchi za Magharibi.

Mtindo wa Kafala umekosolewa sana na masharika yasiyo ya kiserikali na yale yasiyo ya faida. Ripoti ya Kimsingi kutoka Qatar yaonyesha hali ya wafanyakazi wahamiaji, hasa wanaofanya katika miradi mikubwa ya miundombinu wanaohitajika kwa sababu ya Kombe la Dunia, 2022. Ripoti ya Kimsingi ya 2014 inaonyesha changamoto kadhaa katika mtindo huo wa kuajiri.  Mwanzo, bila kujali mikataba ya makubaliano kati ya nchi mbili iliyotajwa hapo awali, mazungumzo haya hutazama ugavi wa kazi na kupuuza pa kubwa mtindo wa kuajiri na mahitaji ya kimaadili. Pili, kama ilivyotajwa awali, wafanyakazi wahamiaji kulipa gharama muhimu za kuajiriwa zifikazo hadi $5,000. Cha tatu, wanakandarasi hulipa makampuni ya usambazaji wa kazi na ajira, badala ya kuwalipa wafanyakazi moja kwa moja, swala linalosababisha hali za uajiri na malipo kuwa za kutatanisha. Hatimaye, kandarasi hizo, iwapo zimetiwa saini, mara nyingi hufichwa kutoka kwa wafanyakazi au kubadilishwa kwa kugeuzwa na malipo ya chini na hali duni zaidi kuliko maelezo yaliyokubaliwa awali. Ripoti hiyo pia inaangazia changamoto kuhusu kuzingatiwa kwa sheria kwa vile vitendo visivyo halali kama uuzaji wa visa bado ni vya kawaida.

Hata hivyo, serikali ya Qatar imeunda mwongozo mpya na wa kujitolea ili kuvunja mtindo wa Kafala, kukijumuisha hatua sita (6) zifuatazo:

  1. Mikataba ya ajira itawekwa na mamlaka ya serikali kwa kuepuka mageuzi na ubadilishaji wa makubaliano hayo, ili kukomesha wafanyakazi kuwasili nchini na kupata mikataba yao imeharibiwa na kubadilishwa na kazi tofauti, mara nyingi za malipo ya chini.
  2. Waajiri hawataweza tena kukataza wafanyakazi wao kuondoka nchini.
  3. Malipo rasmi ya chini zaidi yatawekwa kuwa kiwango cha msingi wa wafanyakazi wote ili kukomesha ubaguzi wa rangi katika mfumo wa malipo.
  4. Makaratasi rasmi ya kujitambulisha yatatolewa na serikali ya Qatar, wafanyakazi hawataweza tena kutegemea waajiri wao kuwapa vitambulisho, hali inayowanyima nafasi za matibabu.
  5. Kamati ya wafanyakazi itaundwa katika kila mahali pa kazi, wafanyakazi kujichagulia wakilishi wao wenyewe.
  6.  Kamati spesheli ya kusuluhisha migogoro ya muda ili kushughulikia malalamiko itakuwa kiundo msingi cha kuhakikisha ufumbuzi wa haraka wa malalamiko.

Pata mengi kuhusu kiwango cha heshima kwa haki za wafanyakazi katika nchi kulingana na ripoti kadirio kuhusu haki za kimaitaifa (ITUC Global Rights Index) hapa.