Ingawa kisheria mashirika ya kuajiri yanatakikana kupata leseni, udanganyifu na matendo mabaya bado yameenea. Kupiga marufuku dhidi ya mashirika ya kuajiri na kuwekeza wafanyakazi kutoka mwaka wa 1995 kuliondolewa tena, kwa vile kuajiri hakungekomeshwa. Ongezeko kubwa la makampuni ya kuhamisha kutokana na sera ya 2005. Sera hiyo ilihitaji makampuni yanayoajiri wafanyakazi wahamiaji chini ya 50 kuajiri moja kwa moja kutoka nchini asili au kutumia makampuni mengine ya kuajiri.  Kwa ajili ya kufanya mtindo wa kuajiri kuwa na ufanisi na rahisi, mfumo huo mpya uliimarika na kuzidi uwezo wa serikali na kusababisha dhuluma kuhusiana na ada za kutozwa. Hii ilisababisha kukatizwa kwa kutoa leseni na vibali vya kazi kwa makampuni ya kuhamisha na kuajiri. Tangia mwaka wa 2013 mfumo wa uhamisho na kuajiri umeondolewa.

Mpango wa Kumi na Moja wa Malaysia unathibitisha mabadiliko katika sera na kusema kwa Wizara ya Rasilmali ya Kibinadamu kuwajibika na kudhibiti kuajiriwa kwa wafanyakazi wahamiaji. Shughuli za makampuni ya kuhamisha na mengine ya maamuzi ya kuajiri zimeondolewa kabisa. Hata hivo, makampuni ya kuhamisha bado wanamiliki leseni zao hadi 2021. Mara nyingi makampuni hayo hayapatiani wahamiaji vifaa vizuri vya malazi, kazi nzuri, uhuru wa kutembea na kiwango mwafaka cha mshahara kisheria.

Bima na huduma za afya zilikua shida kubwa sana kwa wafanyakazi wahamiaji, lakini kutoka mwaka wa 2012 imekua lazima kwa wafanyakazi wahamiaji wote kuwa katika mpango wa hospitali na upasuaji (Hospitalization and Surgical Scheme); malipo kuwa juu ya mwajiri au mwajiriwa. Hata hivo, wafanyakazi wa nyumbani hawahusishwi katika masuala mengi ya kawaida ya ulinzi kikazi, yakijumuisha udhibiti wa masaa ya kazi, siku za mapumziko, likizo, kiwango cha chini cha mshahara kisheria au usalama wa kijamii. Mabadiliko ya hivi karibuni yanapaswa kuimarisha mapato ya wafanyakazi wahamiaji kwa vile waajiri hawafai kukata ushuru kutoka kwa mishahara yao tena.

Pata mengi kuhusu kiwango cha heshima kwa haki za wafanyakazi katika nchi kulingana na ripoti kadirio kuhusu haki za kimaitaifa (ITUC Global Rights Index) hapa.