Maelezo yafuatayo ni ya kijumla kuhusu makubaliano ya kikazi ya nchi mbili ambayo serikali ya Malaysia imetia saini;

Cambodia, 2015; kuhusu kuajiri wafanyakazi, hali ya kuajiri, mkataba wa kazi, muda wa kuajiriwa, mipango ya kifedha.

Cambodia, 2014; kuhusu kuajiri kwa wafanyakazi wa nyumbani wanaotumwa nchini Malaysia.

Indonesia, 2006; kuajiri na kuwekwa kazini kwa wafanyakazi wa nyumbani kutoka Indonesia.

Thailand, 2003; mkataba wa makubaliano kuhusu kazi nchini Thailand.

Vietnam, 2003; makubaliano kati ya nchi mbili kuhusu ushirikiano katika ajira.

India, 2009; mkataba wa makubaliano kuhusu uajiri wa wafanyakazi, ulinzi, na maslahi ya Wahindi nchini Malaysia na hata wafanyakazi wa Malaysia wanaonuia kufanya kazi nchini India.

Bangladesh, 2015; mkataba wa makubaliano kuhusu uuzaji wa nguvu za kikazi nje ya nchi.

Pakistan, 2003; mkataba wa makubaliano kuhusu uuzaji wa nguvu za kikazi nje ya nchi.