Hadithi za wafanyakazi na ukiukwaji wa haki

AHADI AMBAZO HAZIKUTIMIZWA NA PIA MIILI ILIYODHOOFIKA - SAFARI YA MFANYAKAZI WETU MHAMIAJI

Tuliarifiwa na wakala wa uajiri katika kijiji chetu kwamba kazi inapatikana nje ya nchi na mshahara wa dola za Marekani 400 kwa mwezi. Walituambia kazi hiyo ilikuwa katika kiwanda cha karatasi na tutafanya kazi kwa masaa nane kwa siku, siku sita kwa wiki. Wakala huyo alituarifu kwamba hakutakuwa na ada ya kuajiriwa, kwani ingetolewa kutoka kwa mishahara.

Wiki moja kabla ya kuondoka, tulisafiri kwenda mji mkuu kwa mwelekezo wetu wa kabla ya kuondoka. Tuliuliza wakala kuhusu kandarasi yetu lakini tuliambiwa tusiwe na wasiwasi juu yake sasa na kwamba tutapata kabla ya kuondoka.

Kwenye uwanja wa ndege, siku ya kuondoka, tuliulizwa kutia saini kandarasi. Mkataba haukuwa vile wakala alituahidi. Mshahara katika kandarasi hiyo ilikuwa tu $ 200 ya Amerika. Tulipewa pia risiti ya Dola za Marekani 100 kwa malipo ya ada ya kuajiri ambayo tunadaiwa sasa.

Fikiria mshtuko wetu. Lakini hakukuwa na kitu ambacho tunangeweza kufanya kwani tulikuwa kwenye uwanja wa ndege na tayari kwenda. Familia zetu zilikuwa na tumaini kwamba tutaweza kuwasaidia na ajira zetu mpya.

Baada ya safari yetu ndefu ya ndege, tulipofika kwenye ajira zetu mpya, tuliambiwa tusaini kandarasi nyingine na tukaarifiwa kuwa mkataba huu mpya utawasilishwa kwa mamlaka.

Mkataba huu ulisema kwamba tutafanya kazi kwa kampuni ya utengenezaji wa bomba na mshahara wa Dola za Marekani 200 kwa mwezi. Hatukupewa nakala ya mkataba huu, na mwajiri alichukua pasipoti zetu.

Kazi katika kampuni ya utengenezaji wa bomba ilikuwa mbaya sana, na afya yetu ilidhoofika. Tulifanya kazi masaa 10-12 bila malipo ya ziada. Kwa miezi sita ya kwanza, mshahara wetu wote ulilipa ada ya kuajiriwa.

Hundi ya kwanza ya malipo tuliyopata ilikuja baada ya miezi saba ya kazi, lakini ilikuwa tu kwa $ 100 ya Amerika. Tuliuliza mwajiri wetu kwanini tumepokea tu nusu ya mshahara katika kandarasi yetu. Hapo ndipo tukaambiwa kwamba makaazi na gharama za chakula zilikatwa kutoka kwa mishahara.

Hatukuwa na nguvu - tuliuliza mbona mabadiliko, na tukatishiwa kufukuzwa nchini ikiwa hatukujitokeza kazini.

Mwishowe, tuliwasiliana na tukauliza familia zetu nyumbani kuomba shirika la wahamiaji litusaidie. Shirika lilituunga mkono kufungua kesi kwa Wizara ya Kazi . Kupitia msaada wao tuliweza kupata mshahara ulioonyeshwa katika kandarasi yetu.

Migrant workers reporting their case to migrant rights organisation to seek foe help
Migrant workers filed their complaint about their recruitment process to a local union.

KAMA NINGALITUMIA MSHAURI WA UAJIRI, NINGEWEZA KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU WAKALA WA UAJIRI NA JINSI WALIVYO WATENDEA WAFANYIKAZI.

WAFANYIKAZI WENGINE HAWAPASWI KAMWE KUPITIA NILICHOPITIA.

TUMIA MSHAURI WA UAJIRI WA WAHAMIAJI KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU HAKI ZAKO

Kesi hiyo iliripotiwa kwa shirika la Wahamiaji barani Asia na kuandikishwa kupitia utaratibu wa malalamiko ya Hamsa . Hamsa anaruhusu wafanyikazi wahamiaji kuripoti ukiukaji wa haki za wahamiaji na unyanyasaji katika mchakato wa kuajiri. Malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyikazi wahamiaji yatapelekwa na kushughulikiwa na wanachama wa Jukwaa la Wahamiaji huko Asia na vyama vya wafanyikazi. Majina na maelezo yamebadilishwa kulinda mfanyikazi, lakini ukweli unabaki vile vile.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyikazi vya Kimataifa (ITUC) na shirika la Wahamiaji huko Asia wanakuza uajiri wa haki kwa wafanyikazi wahamiaji. Hadithi hizi zitasaidia watu wanaotafuta kufanya kazi nje ya nchi kujifunza kutoka kwa uzoefu wa wafanyikazi ambao wametangulia.

• Shiriki uzoefu wako kuhusu Mshauri wa Uajiri.
• Kadiria wakala wako.
• Jua haki zako.
• Tafuta jinsi ya kupata msaada.

KUFUNGIWA NA BILA CHAKULA

USIYAFANYE MAKOSA NILIYOYAFANYA - TAZAMA Mshauri wa uajiri ili KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSU WAKALA WAKO AU MWAJIRI MTARAJIWA.

Nilitaka kufanya kazi nje ya nchi ili kupata pesa ninazohitaji kutunza familia yangu.

Kuna kazi chache sana mahali ninapoishi, na familia nyingi katika kijiji changu zina jamaa anayefanya kazi nje ya nchi na anawasaidia.

Jirani aliniambia kuhusu nafasi ya kufanya kazi nje ya nchi kama mkulima kwa dola za Marekani 300 kwa mwezi. Niliambiwa kazi hiyo haikuwa ngumu na inanipa pesa za kutosha kutuma kwa familia yangu.

Nilimlipa wakala Dola za Marekani 600 kwa ahadi ya kazi hii.

Mwezi mmoja kabla ya kuondoka, nilimuuliza wakala kuhusu kandarasi yangu na idhini ya kufanya kazi, na niliuliza ikiwa virusi vya corona vitaathiri kazi yangu. Nilikuwa nimesikia kuhusu virusi vya corona kwenye habari. Wakala alisema hakukuwa na virusi vya corona katika nchi ninayokuwa nakwenda na nitasaini mkataba kabla ya kuondoka.

Siku ya kuondoka, niliulizwa kutia saini kandarasi, lakini ilisema kwamba mshahara wangu ungekuwa Dola za Marekani 200 kwa mwezi.

Sikutaka kusaini, lakini nilihisi ni lazima kwa sababu nilikuwa tayari nimelipa Dola za Marekani 600 kwa wakala huyo. Pia, nilimwuliza wakala risiti ya ada ya uajiri na nikapatiwa risiti ya Dola za Marekani 100, ambayo ndiyo ada ya juu inayoruhusiwa katika nchi yangu.

Nilipofika mahali nilipokuwa nikienda, nilikutana na wakala mwingine na kuulizwa nisaini mkataba mpya. Lakini sikupewa nakala ya mkataba, na pasipoti yangu ilichukuliwa na mwajiri wangu.

Nilipofika mahali pa kazi, niligundua kazi ilikuwa katika ujenzi, sio bustani. Nililazimika kufanya kazi hadi masaa 12 kwa siku kwa mwezi na sikulipwa chochote.

Sikuwa na makaazi sahihi na ilibidi nishiriki chumba kimoja na wafanyikazi wengine 15 karibu na eneo la ujenzi.

Baada ya miezi miwili, tuliambiwa kwamba ujenzi utasimama kwa sababu serikali imeanzisha karantini ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Hatukuruhusiwa kuondoka kwa makao yetu kwa wiki tatu, na tulikata tamaa kwa sababu kampuni hiyo iliacha kutupatia chakula.

Hatukuweza kwenda nje kutafuta chakula kwa sababu polisi wangetuweka kizuizini kwa kuvunja karantini.

Tulilazimika kuchapisha picha za hali yetu kwenye Facebook na kuomba msaada.

Migrant workers from different origin countries about to return home after seeking help for repatriation
Migrant workers from different origin countries were waiting for the repatriation process

KAMA NINGALITUMIA MSHAURI WA UAJIRI, NINGEWEZA KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU WAKALA WA UAJIRI NA JINSI WALIVYO WATENDEA WAFANYIKAZI.

WAFANYIKAZI WENGINE HAWAPASWI KAMWE KUPITIA NILICHOPITIA.

TUMIA MSHAURI WA UAJIRI WA WAHAMIAJI KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU HAKI ZAKO

Kesi hiyo iliripotiwa kwa shirika la Wahamiaji barani Asia na kuandikishwa kupitia utaratibu wa malalamiko ya Hamsa . Hamsa anaruhusu wafanyikazi wahamiaji kuripoti ukiukaji wa haki za wahamiaji na unyanyasaji katika mchakato wa kuajiri. Malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyikazi wahamiaji yatapelekwa na kushughulikiwa na wanachama wa Jukwaa la Wahamiaji huko Asia na vyama vya wafanyikazi. Majina na maelezo yamebadilishwa kulinda mfanyikazi, lakini ukweli unabaki vile vile.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyikazi vya Kimataifa (ITUC) na shirika la Wahamiaji huko Asia wanakuza uajiri wa haki kwa wafanyikazi wahamiaji. Hadithi hizi zitasaidia watu wanaotafuta kufanya kazi nje ya nchi kujifunza kutoka kwa uzoefu wa wafanyikazi ambao wametangulia.

• Shiriki uzoefu wako kuhusu Mshauri wa Uajiri.
• Kadiria wakala wako.
• Jua haki zako.
• Tafuta jinsi ya kupata msaada.

Woman migrant domestic worker filling in a complaint form
Migrant domestic worked filed a complaint to a local organisation about her recruitment agency and employer.

KUWEKWA PEKEE, KUACHWA NA NJAA NA KUPIGWA
 
Mume wangu ni kipofu, kwa hivyo mimi ndiye pekee katika familia yangu ambaye angeweza kufanya kazi, na sikuweza kupata pesa za kutosha kutunza familia yangu katika nchi yangu ya nyumbani.

Nilikuwa nikifanya kazi ya kusafisha nyumba, nikienda kwenye nyumba mara tatu kwa wiki na kufulia familia mbili. Nilikuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi, lakini bado familia yangu ilihitaji nipate zaidi.

Ndipo nikasikia kutoka kwa jirani kwamba kulikuwa na dalali katika kijiji chetu ambaye alikuwa amewasaidia watu katika jamii yetu kupata kazi nje ya nchi.

Dalali aliniahidi kazi na mshahara wa Dola za Marekani 300, ambazo zingetosha kutuma pesa nyumbani, lakini nililazimika kulipa ada ya uajiri ya Dola za Marekani 750. Dalali alisema kuwa ada hiyo italipa visa yangu, ndege, ukaguzi wa matibabu na mafunzo.

Ili kupata pesa za ada, tulilazimika kuweka rehani shamba letu dogo la familia.

Nililipa ada na kuambiwa nitaondoka baada ya miezi mitatu. Nilipata pasipoti na uchunguzi wa kitabibu, lakini hakukuwa na mafunzo au mwelekezo wa kabla ya kuondoka

Siku mbili kabla ya kuondoka, nilisafiri kwenda mji mkuu na nikakaa katika ofisi ya wakala wa uajiri. Pale ofisini waliniuliza nisaini kandarasi, ambayo sikuweza kuelewa kwa sababu ilikuwa katika lugha ambayo sijui.

Nilisafiri na wanawake wengine kumi, wote wakiwa wafanyikazi wa nyumbani. Tulipofika katika hio nchi nyingine, tulienda moja kwa moja kwenye nyumba ambazo tutafanya kazi. Hakuna mafunzo au mwelekezo wa kabla ya kazi.

Kazi niliyopaswa kuifanya ilinichosha kabisa . Nilikuwa nikifanya kazi katika nyumba tatu tofauti, kwa masaa kumi na tano kila siku, nikipika na kusafisha kwa familia. Sikujawahi kupata siku ya kupumzika na sikuruhusiwa kutumia simu ya rununu kuwasiliana na familia yangu

Hii iliendelea kwa miezi mitatu, na kuzidisha ubaya zaidi, hata sikulipwa. Katika mwezi wangu wa nne, nilimuuliza wakala wa uajiri kunihamisha; kufanya kazi katika nyumba tatu ilikuwa ni nyingi sana

Kisha unyanyasaji wa kimwili ulianza. Nilihamishiwa kwa mwajiri mpya ambaye angenipiga na kunipa chakula kidogo sana, na nilikuwa bado nikifanya kazi masaa mengi bila siku ya kupumzika.

Baada ya miezi mitano mwishowe nililipwa, lakini niliogopa; Nilipewa dola za Marekani 150 tu. Mwajiri wangu aliniambia kuwa hii pesa ndio ilikubaliwa na wakala wa uajiri.

Miezi kumi baada ya kufika, nilikuwa nimekata tamaa na niliogopa, na niliwasiliana na shirika linalosaidia wafanyikazi wahamiaji. Singeweza kuvumilia unyanyasaji tena. Nilikuwa mwembamba na mwenye njaa na nilikuwa na michubuko mikononi na mgongoni mwangu.

KAMA NINGALITUMIA MSHAURI WA UAJIRI, NINGEWEZA KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU WAKALA WA UAJIRI NA JINSI WALIVYO WATENDEA WAFANYIKAZI.

WAFANYIKAZI WENGINE HAWAPASWI KAMWE KUPITIA NILICHOPITIA.

TUMIA MSHAURI WA UAJIRI WA WAHAMIAJI KUPATA HABARI ZAIDI KUHUSU HAKI ZAKO

Kesi hiyo iliripotiwa kwa shirika la Wahamiaji barani Asia na kuandikishwa kupitia utaratibu wa malalamiko ya Hamsa . Hamsa anaruhusu wafanyikazi wahamiaji kuripoti ukiukaji wa haki za wahamiaji na unyanyasaji katika mchakato wa kuajiri. Malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyikazi wahamiaji yatapelekwa na kushughulikiwa na wanachama wa Jukwaa la Wahamiaji huko Asia na vyama vya wafanyikazi. Majina na maelezo yamebadilishwa kulinda mfanyikazi, lakini ukweli unabaki vile vile.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyikazi vya Kimataifa (ITUC) na shirika la Wahamiaji huko Asia wanakuza uajiri wa haki kwa wafanyikazi wahamiaji. Hadithi hizi zitasaidia watu wanaotafuta kufanya kazi nje ya nchi kujifunza kutoka kwa uzoefu wa wafanyikazi ambao wametangulia.

• Shiriki uzoefu wako kuhusu Mshauri wa Uajiri.
• Kadiria wakala wako.
• Jua haki zako.
• Tafuta jinsi ya kupata msaada.

Migrant Forum in Asia (MFA)

Conceived in 1990 in a meeting of migrant workers’ advocates in Hong Kong, MFA was formally organized in 1994 in a forum held in Taiwan entitled, “Living and Working Together with Migrants in Asia”.

MFA is a regional network of non-government organizations (NGOs), associations and trade unions of migrant workers, and individual advocates in Asia who are committed to protect and promote the rights and welfare of migrant workers.

http://mfasia.org

International Trade Union Confederation (ITUC)

The International Trade Union Confederation (ITUC) is the global voice of the world’s working people.

The ITUC’s primary mission is the promotion and defence of workers’ rights and interests, through international cooperation between trade unions, global campaigning and advocacy within the major global institutions.

https://www.ituc-csi.org